Jifunze kuhusu Uagizaji

Jinsi ya Kuingiza Bidhaa

Ushuru hutozwa kwa bidha zozote zinazoingizwa na kuondolewa nchiini kabla kuzitoa kwa forodhani;Isipokuwa bidhaa zinazostahili upendeleo maalum kwa mujibu wa sheria na kanuni,ambapo ushuru umesamehewa.

Ili kuingiza bidhaa kama gari au mashine unahitaji kuhusisha wakala wa ushuru na forodha.

 

Unapohusisha wakala wako unayemchagua hakikisha una:

  • Fomu ya tangazo ya kuingiza bidhaa (IDF)
  • Fomu ya kiingilio ya forodha (Customs Entry)
  • Cheti cha utimilifu (CoC) kutoka kwa wakala wa PVoC kwa bidhaa zinazodhibitiwa
  • Kiwango gezi cha kuingiza bidhaa kinapohitajika
  • Ankara halali ya kibiahsara kutoka kwa shirika la uondoshaji wa bidhaa
  • Ankara kadiria(proforma) kutoka kwa shirika la uondoshaji

 

Wakala wa ushuru wa forodha anaruhusiwa kutangaza bidhaa anazoingiza kwenye mifumo mbalimbali ya forodha.